Home WETU

WETU

Ndio, lugha, tunazo nyingi.
Neno zingekuwa shillingi,
Tungekuwa sote matajiri.

Tusijilinganishe na mti,
Mwenye tunamuona kwa runinga,
Ati matawi zake na zangu zafanana rangi.
Jilinganishe na Jirani.
Mwenye anaeza kutunza watoto,
Tukienda kazi.
Siku ijayo, nikikosa.
Ndiye atanisaidia chumvi.

Bega kwa bega,
Tunayo nguvu ya kuhakikisha uhai ya amani.
Tusikubali kuwa nyasi,
Ndovu zikipigania Udume.
Vijana tuungane, wewe na mimi,
Ili kesho tukule, leo, tulime.

@RayaWambui

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Subscribe to our newsletter

Click Subscribe to get our latest news and stories straight to your email