Jadi nilipokupenda,
wakti lolote ningetenda,
ahadi ulipanda,
nkatarajia kuvuna,
hisia na huba,
farha si haba,
kumbe haba na haba,
haujazi kibaba bin riba, loh!
Longo longo,
jicho la moyo nalo chongo,
sikujua ni hongo,
penzi ulonipa,
heri ngetia usongo,
nsipumbazwe na udongo,
umenifunza hata kwa matongo,
samaki humjua papa !!
Dalili ulinipa,
ila macho nilifumba,
ulinifunga kwa kamba,
nami maskio nkatia pamba,
kama damu kwa mshipa,
nilikuthamini mahabuba,
sikujua wetu usuhuba,
ni mazigazi ya jangwa, loh!
Longo longo,
jicho la moyo nalo chongo,
sikujua ni hongo,
penzi ulonipa,
heri ngetia usongo,
nsipumbazwe na udongo,
umenifunza hata kwa matongo,
samaki humjua papa !
Ulinihadaa, nami nilikaa,
kijipa tumaini, ukanikeketa maini,
ulinikalfisha, ila mda wako umekwisha,
mbio za sakafuni, huishia ukingoni,
Click on the poet’s name to view his blog
courtesy of Storyzetu
4 Responses
Kibali pia Kiswahili akitambua
haha naishi mombasani, ndio lugha yetu 😀
I’ve read a whole shairi word for word. Someone give me a medal! Whether I’ve understood it is a different story all together.
Wait, I was supposed to comment in Swahili right?
Nimesoma shairi nzima neno kwa neno. Nipatieni nishani…….
Kibali Longo Longo sasa ni nini?
Whoa! Kumbe mashairi bado yanatia fora?! I luv swa poetry n sana sana the rhyme of ths poem. Really catchy!