Home BARUA LA MWISHO.

BARUA LA MWISHO.

image

“Mpenzi wangu halima.
Imekuwa siku mingi tangu tuongee Ana kwa Ana.hata kama ni salamu tu kwenye radio mimi ningeridhika na moyo wangu ungetulia. Tangu ile siku ya harusi ya omar sijui kaenda wapi.hata barua hino najua hutalipata inaweza kuwa mussa kanichezea shere ati “halima Yule kidosho kamcheki kuleee ……..”kawaida ya mussa hayo.

Lakini yangu sio mateta Ila tu kusema kwaheri.kwani barua hili ni barua langu la mwisho.usidhani kwamba hela sina.hapana. pesa n’nazo. Lakini ijapokuwa pesa nimepata haliwezi n’nunulia penzi lako. Ndiposa moyo kajawa machungu. Hujaitika nyaraka zangu zingine wala hujadhubutu kun’tumia hata moja.basi mbona niishi tena? Maadam naona hunipendi tena.mbona halima Ilhali wajua mdundo wa penzi lako ndio mdundo wa roho yangu. Halima. Barua hii ni ya kwaheri.kwaheri ya milele sababu kitambo usome hii ntakuwa nanywa sharubati mbinguni. nakupenda halima ”

“Mpenzi juma.mbona machungu.penzi langu kwako halijafifia lakini tangu harusi imenibidi nikutoroke.usidhani kwamba wewe ndiye mwenye kosa.la hasha. Ni mimi mtenda dhambi hapa.

Wakumbuka usiku ya mwisho wa January?uliponepeleka chumbani mwako?jinsi ulivyonishika, ulivyoniimbia na kunibusu? Usiku huo Ulikuwa mtamu sikatai. Kusema kweli wewe ni mtema kuni mwenye vipawa. Lakini ni usiku huo ulibidi nitoroke nilipogundua niko na mimba yako.Ilibidi niende la sivyo sote tungelaaniwa na jamii. Juma jameni usijiue maadam una mtoto jina mustafa.juma tafadhali baki.twakupenda juma.”

Juma hakupata barua ya halima.iwapo aliiona basi aliionea mbinguni akinywa sharubati……

0 Responses

  1. Ngartia says:

    suspense Maaaan!! suspense … I’m pretty sure many of the readers didn’t read to the end. Do you have to tell us straight that the guy committed suicide?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Subscribe to our newsletter

Click Subscribe to get our latest news and stories straight to your email

Hello

Subscribe to our newsletter