Home Apocalypse

Apocalypse

“I wanna live forever young, do you wanna live forever?”
Ambia JayZ kaburi ni jumba lake la maisha,
‘Cause ya ulimwengu yataisha,
Smile zitaboeka, beauty itazoeka,
Watabomoa ukuta na kisha watajenga ufa, uhai utakufa.
Mapenzi itachukia,
Kwa world dhambi itakua na ufalme na kifo itakua malkia.
Wanyama watagive birth to binadamu,
Chuki itatabasamu,
Science itacreate immorality na humans watalipia oxygen.
Kuishi itapoteza hamu, binadamu watatuma “Please call me” kwa Mungu
Binadamu watataka kutoa tithe na pesa zao zitakataliwa mpaka na ma beggar.
Watawish kupata mtu wa kuwatolea uzito kwa mabega.
Makanisa zitakua na ma bouncer kwa mlango wakichagua,
Wakiwa na alcohol blow na ma bomb detector wakikagua.
Time inakam,
Time inakam when celebrities na ma Role models watakua brand ya kumarket na kusell usherati na dhambi.
Time inakam,
Time inakam kuna prophet mwenye atazaliwa ghetto ndani ya nyumba ya bangi na veve.
Niko among hao maprophet wenye watakam na nitainga hao ma pastor wa uwongo na ma biashara njere,
Niko among hao maprophet watakam wakibonga na sheng’,
Niko among hao ma prophets wenye watakam wa dreadi ndio words zangu zifikie hao wenye hii smoke ma pushupeng.
Time inakam when hata makaburi zitakataa gereza,
Binadamu watakunywa na kikombe ya Ebenezer,
Prayer ya Paulo na Sila zitawaweka kwa Gereza,
Wawe kwa grass root kama Nebuchadnezzar,
Words spiritual zitasambaza upele,
Makucha zitamea nywele,
Silence itapiga kelele,
Sssssh!
Movements zitastand still.

God niko stainless still,
A minute of silence, Holy Spirit anahunt for souls ziko stainless.
Death hucelebrate birthday the moment sin huwa committed kama suicide,
Time ilikuwa inakam sasa imefika,
Dhambi imeshawanajisi; sasa wamebeba mimba ya ibilisi.
Uchungu na uzito wa kumlea mwana ndio sasa wanahisi,
Watacelebrate ukikoma kuishi,
Kwa birthday yako wanaimba nyimbo za mazishi,
Wanablow out candle zinanuka moshi ya weed,
Wanakata keki inableed,
Ukahaba, kuvunjwa ubikra,
kisha wakazini kimawazo hisia, jinsia na fikira,
Bibilia husema itapipiquwa Iqra.
Kifo itashika mimba, na kisha itazaana,
Mtoto wake 1st born ataitwa laana na last born atapoteza maana,
Curses zitarule!
Mablessing zitakua overpowered, bravery itakua coward,
Don’t wish to see tomorrow, ‘cause tomorrow is so painful,
Tomorrow joy will get married to sorrow,
Na Adam ataignore Eve aget married na serpent,
Tomorrow Human watakua Evil servants,
Tomorrow Abel na Cain watazini na wazae Avatars,
Tomorrow kutakua na unabii wa uwongo but chenye najua is that kwa pulpit ya Heaven kila pastor ni amateur,
Tomorrow ukweli itasema uwongo, kipofu ataongoza chongo kwa wenye macho walishaonyesha God mgongo.
World itakua full of hatred na 14th Feb itakua omitted kwa calendar,
Heaven kila mtu ataingia na suti, sio zenye alizikwa nazo but zenye alizaliwa nazo,
Bible ishaitwa old fashioned, ukuta za altar zimecrack, Bibles zina cobwebs, church zimewachiwa mashosho na wazee,
Mayouth wanafellowship vimaximum kwa prison na mahospitali,
Wototo wanataka kugrow into maceleb,
Generation yenye macho nzito na wanawatch uchafu kwa web,
Hakutakuwa na vita tena, but the battle itakua deep within,
Human heart, conscious na consequences za sin.

© Tear Drops

3 Responses

  1. Joseph Mutiso says:

    This is massive. Big up Tear drop 💧

  2. Gnazz titan says:

    hio inaguza ndipo. tunataka izi realty zimefichwa but zimejichora mtaani.. 👊

  3. I also love poetry na ur my mentor tangu nianze kuona ur poets churchil show manze ulinijaz thenks naomba unisaidie kunifunza more

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Subscribe to our newsletter

Click Subscribe to get our latest news and stories straight to your email

Hello

Subscribe to our newsletter